Niyonzima ni levo za kina Lunyamila?
Na Samuel Samuel
Wana Dar Young African wana deni na mtu huyu. Wapo wachezaji waliopita ndani ya Jangwani na kuitendea haki nafasi ya kiungo mchezeshaji na kuacha alama za miguu yao ndani ya vifua vya wana Dar Young Africans.
Wachezaji kama Method Mogela , Said Mwamba " Kizota" na hata Salvatory Edward achilia mbali Athuman Idd. Utake usitake malazi yaliyomkumba Niyonzima mwishoni mwa msimu uliopita yalichangia sana Yanga kuukosa ubinga.
Unapomzungumzia Haruna Niyonzima, unaizungumzia roho ya Yanga kwa sasa katika kutawanya mipira kule mbele, ndiye kiungo anayekubali mifumo yote ya mwalimu kutokana kipaji alichonacho cha kubadilika kutokana na mazingira na uwezo wa kupambana na msitu wa wachezaji wa timu pinzani na yeye kubaki katika ubora wake.
Ikumbukwe pia ni Nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda. Hawakukosea kumpa. Ni kiongozi ndani ya uwanja na nje ya uwanja kutokana na nidhamu nzuri ya soka na binafsi. Niyonzima ataibeba yanga vizuri octoba 18 kama Maximo atampanga kama kiungo huru ( free midfielder) .
Ana uwezo wa kucheza vizuri akiwa nyuma ya fowadi lines na kutamba angle zote kutokana na stamina, ufundi wa kumiliki mpira hata kutengeneza nafasi. Anakuwa imara zaidi akianza na Ngasa , Msuva, Dilunga na Nizar Khalfan.
Wote hawa anajua jinsi gani ya kucheza nao kutokana na kasi yao ili kule mbele Kukae katika mfumo hatari kimashambulizi. Yanga ina deni na mtu huyu.
Anahitaji kuingia katika orodha ya legends wa Yanga kama kina Costantine Kimanda, James Tungaraza , Lunyamila na wengine.
0 comments:
Post a Comment