Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 October 2014
Friday, October 17, 2014

Uchambuzi: Arsenal vs Hull City


Na Chicoti Cico


Washika bunduki wa jiji la London timu ya Arsenal wataikaribisha Hull City kwenye uwanja wao wa Emirates huku kocha Arsene Wenger akikabiliwa na wachezaji wengi majeruhi. Arsenal inatarajiwa kuwakosa mabeki Laurent Koscielny, na Calumn Chambers anayetumikia adhabu. 

Pia Arsenal itawakosa viungo wake Mesut Ozil, Aaron Ramsey na Serge Gnabry huku washambuliaji Olivier Giroud na Yaya Sanogo nao pia watakuwa nje wote huku habari njema kwa Arsenal ikiwa ni kurejea kwa Mikel Arteta aliyekuwa majeruhi.

Mpaka sasa timu ya Arsenal haijashinda mchezo wowote wa ligi nyumbani huku wakicheza michezo miwili na kutoka sare dhidi ya Manchester City na Tottenham Hotspur hivyo washika bunduki hao wa London watapigana ipasavyo kuweza kutafuta ushindi wa kwanza nyumbani toka kuanza kwa ligi.

Arsenal ambao wanashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 10, wamekuwa na mwanzo mbovu kwenye msimu huu wa ligi huku wakishinda michezo miwili na kutoka sare michezo minne na kupoteza mchezo mmoja kati ya michezo 7 tangu ligi kuanza.

kwa matokeo hayo kocha Wenger atataka kushinda dhidi ya Hull City ili kuondokana na wimbi la sare lakini pia kupunguza “gap” dhidi ya vinara Chelsea.

Hully City wanaofundishwa na kocha Steve Bruce wana wachezaji wawili majeruhi wa muda mrefu ambao ni kipa Allan McGregor na Robert Snodgrass ambao hawatacheza dhidi ya Arsena.

Mohamed Diame akiangaliwa kama ataweza kuanza kutokana na uchovu wa safari wakati akiitumikia Senegal kwenye michezo ya kimataifa.

Mpaka sasa Hull City wanashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama tisa huku wakiwa wameshinda michezo miwili, kutoka sare michezo mitatu na kupoteza michezo miwili.

Hivyo tofauti ya alama moja kati ya Arsenal na Hull City inamfanya kocha Steve Bruce kuingia kwenye ya leo kwa nguvu zote kutafuta ushindi wa tatu na kujitengenezea mazingira mazuri kwenye ligi. 

Rekodi kati ya Arsenal vs Hull City zinaonyesha kwa pamoja wamecheza michezo 13 huku Arsenal akishinda michezo 10 na Hull City akishinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!