Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 October 2014
Friday, October 17, 2014

Uchambuzi: Crystal Palace vs Chelsea


Na Chikoti Cico


Chelsea wanarejea tena kwenye uwanja wa Selhurst Park wakiwa na kumbukumbu mbaya ya msimu uliopita baada ya kufungwa kwa goli 1-0 na Crystal Palace moja ya matokeo yaliiyomnyima ubingwa kocha Jose Mourinho.

Nahodha wa Chelsea John Terry ambaye alijifunga mara ya mwisho walipokutana na Crystal Palace msimu uliopita, ataweka rekodi mpya kwenye mchezo huo kwa kufikisha michezo 500 kama nahodha kwenye klabu ya Chelsea toka alipopewa unahodha msimu wa mwaka 2004/2005.

Chelsea wanaongoza ligi kuu ya Uingereza kwa jumla ya alama 19 huku mpaka sasa, wakiwa hawajapoteza mchezo wowote toka ligi imeanza.

Watatamani kuendeleza wimbi la ushindi na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaaa ubingwa ili kutokurejea makosa ya msimu uliopita.

Chelsea wana hatihati ya kuwakosa baadhi ya wachezaji ambao ni majeruhi kama Didier Drogba, Obi Mikel, Ramires na Schurrle huku mshambuliaji wao hatari Diego Costa akitarajiwa kuanza pamoja na kuwa anasumbuliwa na majeraha ya goti.

Chelsea mpaka sasa hawajapoteza hata mechi moja kati ya 10 walizocheza kwenye ligi kuu ya Uingereza huku wakishinda michezo minane na kutoka sare michezo miwili.

Hii ni rekodi ambayo watataka kuiendeleza kwenye mechi ya leo dhidi ya Palace. Huku mshambuliaji wao Diego Costa akiongoza kwa ufungaji akiwa na magoli tisa, kiungo Fabregas akiongoza kwa utengenezaji wa magoli kwa “assists” saba mpaka sasa.

Crystal Palace wanaofundishwa na kocha Neil Wanorck watamkosa beki wao Scott Dann aliyeko majeruhi na baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa na Hull City kwa magoli 2-0, Palace watatamani kushinda dhidi ya Chelsea ili kuondoka nafasi ya 15 waliopo sasa kabla hawajateremka zaidi kwenye hatari ya kushuka daraja.

Kocha Wanorck anatafuta ushindi wake wa pili nyumbani hasa baada ya kupoteza michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja kati ya michezo mitatu Palace waliocheza kwenye uwanja wao wa Selhurst Park huku wakiwa na kumbukumbu nzuri nyumbani ya kuifunga Leicester City kwa magoli 2-0 mwishoni mwa mwezi wa tisa

Rekodi zinasema kwa pamoja Chelsea wamekutana na Crystal Palace mara 35 huku Chelsea wakishinda michezo 15 na Crystal Palace kushinda michezo 6 na wote wakitoka sare michezo 14.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!