Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 October 2014
Thursday, October 16, 2014

Sare na kufungwa kwa Simba SC huko South Africa



Na Samuel Samuel

Sare na kufungwa kwa Simba SC huko South Africa na matokeo ya ligi ya nyumbani kunazidi kuwatoa wachezaji, viongozi na wapenzi wa timu hiyo katika hali ya kujiamini. 

Kiufundi Walinzi wa timu huimarika pale wanapoweza kusahihisha makosa yao lakini wanavyoruhusu kufungwa mara kwa mara, huathirika kisaikolojia na mwisho wa siku wanafanya kazi under pressure. 

Simba imetoa droo ya 2-2 na Coastal Union, ikatoa sare ya 1-1 na Polisi Moro, ikatoa droo tena na Stand United ya 1-1. Hapo ukiangalia wameruhusu kufungwa mfululizo. 

Katika maandalizi ya kuwavaa Yanga hapo Jumamosi, wametoka suluu ya 1-1 Orlando Pirates kabla ya kufungwa 4-2 na jana, wamecheza tena na Jomo Cosmos na kufungwa 2-0. 

Kwa hali hii timu inakosa chemistry sahihi ya soka. Itazame Man U chini ya Moyes , ilikuwa inapata vipigo na sare mfululizo na mwisho wa siku ikaishia nafasi ya Saba. 

Katika maandalizi ya Ligi , Simba imecheza mechi nyingi za kirafiki, Swali je? Makocha wa timu hii wanapata wapi muda wa kuisuka timu? Wanapata kweli muda wa kutengeneza coordination ya timu kama unakuwa na mechi za majaribio za mfululizo?. 

Kocha unatakiwa upate muda wa kutosha kutengeneza mfumo wako huku ukiisoma saikolojia ya wachezaji wako nje ya tension ya mechi. 

Mechi za kirafiki ni muhimu katika kupima uwezo wa timu lakini kama kocha unatakiwa upate muda wa kutosha kuiandaa timu kuliko kukimbilia kuipima timu yako kwenye dakika 90 kila siku. 

Simba inahitaji muda mwingi wa kufanya mazoezi na kuwajenga wachezaji kisaikolojia hasa back lines. Pia wengi wanaweza kuwa wanailaumu back line ya Simba kushindwa kujenga mfumo mzuri wa kujilinda.

 Simba kwa sasa inajengwa na viungo wachezeshaji wengi kuliko wakabaji. Ndemla, Kiemba, Okwi, Singano, Uhuru selemani, Kisiga , wote hawa kiasilia si wakabaji bali ni free midfielders, hivyo basi timu ikipoteza mpira tension yote inarudi nyuma kwa mabeki. 

Phiri anahitaji kutengeneza wakabaji wengi mbali na Mkude na Kwizera. Timu yote inatakiwa iwe na uwezo mzuri wa kujenga mashambulizi na kujilinda pia.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!