Paul Scholes aipa Chelsea ubingwa wa Uefa.
Na Rossa Kabwine
Paul Scholes amesema leo kuwa, Chelsea ndio timu pekee ambayo inaweza kushinda champions league msimu huu. Legendary wa Manchester United Paul Scholes ametumia maneno matamu kuzungumza kuihusu klabu ya Chelsea kwenye mtandao wa standard.co.uk
Baada ya mechi za klabu bingwa barani Ulaya wiki hii, Scholes alichambua utendaji wa timu za Uingereza. Alisema Liverpool imekuwa katika kiwango kibaya, pia alisema ina onekana wametetereka sana kumkosa Luiz Suarez kuliko ilivyo tarajiwa.
Mchazaji huyo wa zamani wa mashetani wekundu alisema kuhusu kuwa, katika timu za Uingereza ni timu moja tu ambayo ina uwezekano wa kushinda kombe hilo nayo ni Chelsea.
0 comments:
Post a Comment