David Luiz: kuondoka Chelsea ilikuwa ni uamuzi wangu
Na Rossa Kabwine
Mlinzi wa PSG alisisitiza kuwa hakuna matatizo kati yake na meneja wake wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho. Mchezaji huyo wakimataifa wa Brazil aliye nunuliwa kwa dau la poundi milioni 50, aliweka rekodi ya kuwa beki mwenye thamani kubwa duniani.
Beki huyo alisema uamuzi wa kuondoka Chelsea haukusababishwa na uhusiano uliokuwepo baina yake na meneja wake, Mourinho. Kama ilivyonukuliwa katika mtandao wa skysports alisema “ ilikuwa chaguo langu, maisha yangu na chelsea yalikuwa yamemalizika. Niliamua kuondoka na kujiunga na klabu ya PSG ambayo walinionesha nia ya kunihitaji"
Luiz ameendelea kubainisha kuwa, Chelsea walikuwa tayari kumpatia mkataba mpya lakini akaona ni bora aondoke na kujiunga na wababe hao wa ligi kuu nchini Ufaransa.
Klabu ya PSG kwa sasa ina alama 18 baada ya kushuka dimbani mara 10 huku wakifunga mabao 18 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara saba pekee.
0 comments:
Post a Comment