Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 October 2014
Sunday, October 26, 2014

Mzimu bado unamuandama Mario Balotelli.


Na Rossa Kabwine

Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, bado hakuwa na mchezo mzuri wakati timu yake ilipotoka sare na Hull City kwenye dimba la Anfield weekend hii.

Balotelli aliendelea kukosa magoli ya wazi kabisa na kufanya presha kutoka kwa mashabiki na media kuzidi kuwa kubwa upande wake. Alikosa goli baada ya kazi nzuri muda wa majeruhi, huku wana Liverpool wakishuhudia mashuti yake mengine yaliokolewa.

Mlinzi wa kati wa Liverpool, Dejan Lovren naye alipiga kichwa lakini mpira uliweza kuokolewa ukiwa kwenye mstari wa goli na mchezaji wa Hull city Ahmed Elmohamady.

Kiungo wa Hull City, Jake Livermore alipoteza nafasi nzuri kabisa baada ya kupiga shuti lilio mlenga kipa wa Liverpool, Simon mignolet.

Bado kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers ameendelea kumuamini Balotelli ambaye hivi karibuni alikosolewa mno na media za Uingereza kutokana na tukio lake la kubadilishana jezi na mlinzi wa Real Madrid, Pepe wakati wa mapumziko.

Matokeo hayo yana maanisha Liverpool, ambao walishika nafasi ya pili msimu uliopita wapo nyuma ya point nane dhidi ya vinara wa ligi hiyo Chelsea ambao wamecheza mechi pungufu Lakini Liverpool walifanikiwa kutokuruhusu goli (clean sheet) kama meneja wao Rogers alivyotaka hivyo kupata clean sheet ya pili msimu huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!