HARUNA NIYONZIMA VS AMRI KIEMBA
Na Samuel Samuel
Katika mechi ya juzi kati ya Taifa Stars na Benin, Amri Kiemba " baba Shabani" alionesha uwezo mkubwa kama kiungo huru pale mbele akishirikiana vizuri na Mwinyi Kazimoto.
Amri Kiemba ana uwezo mzuri wa stamina na pumzi ya kutosha kuzunguka kila kona pale mbele hali hiyo itawafanya mabeki wa Yanga wawe busy muda wote kumchunga mchezaji huyu.
Wakati Amri aking'ara kwenye mechi hiyo na kutoa ishara ya hatari juu ya Yanga, Maximo naye anakifaa Haruna Niyonzima ambaye toka Ngao ya hisani na mechi zote za ligi ameonesha uwezo mkubwa kuiunganisha timu kule mbele kama kiungo mchezeshaji.
Simba inaweza ikaanza hivi Nafasi ya ulinzi , Golini akisimama Casilas, full back right akipewa Chollo maana ni mkongwe ndani ya Simba na anajua pressure za watani, kushoto Baba ubaya kama Full back left.
Baba ubaya ndie beki ambaye Phiri ana imani naye 100% ana uwezo mzuri wa kuzuia na kupanga mashambulizi. Half back four akisimama Mgeveke, kijana ni chipukizi na Simba walimtoa timu ya maji maji baada ya kumuona akifanya yake na timu ya taifa ya maboresho.
Mgeveke ni mechi yake ya kwanza dhidi ya Yanga lakini bado ni beki mzuri mwenye uwezo wa kuwachachafya washambuliaji hatari wa yanga kama Jaja, Msuva na Mrisho Ngasa.
Sentafu bila shaka Phiri atamsimamisha Owino. Nafasi ya viungo, Phiri anaweza kuja vingine akiitazama Yanga ya Maximo inayotumia mfumo wa 4-5-1 ikijaza viungo wengi kati hivyo Phiri anahitaji kuweka watu wa kazi akitaka kuimiliki ngome hiyo.
Badala ya kumpanga Jonasi Mkude kama kiungo mkabaji, atampanga Piere Kwizera mwenye kasi na uwezo mzuri wa kutoa squre pasi ili Jonas Mkude akamsimamishe kama kiungo mshambuliaji .
Mkude ana nguvu na uwezo mzuri wa mashuti. Phiri atatamani kumpanga nafasi hiyo Mkude baada ya Jabir Aziz wa Kuufunua udhaifu wa Deogratius Munish "Dida" kucheza mashuti ya mbali.
Jabir Aziz alimtungua Dida umbali wa mita 34 mechi kati ya Yanga na Ruvu JKT. Said Ndemla, kijana mrefu na mwenye uwezo mzuri wa kukaba na kasi anaweza kupanga kama winga wa kulia huku Uhuru Selemani Akitokea benchi.
Ndemla ikumbukwe alichangia kwa kiasi kikubwa kubadili matokeo mechi ya mtani jembe msimu uliopita. Yanga ilikuwa ikiongoza 3-0 mpaka half time.
Lakini kipindi cha pili alipoingia Ndemla aliiwezesha Simba kutulia na kupiga pasi nzuri na kuzawazisha magoli yale. Winga ya kushoto Phiri ana uamuzi aidha kumpanga Ramadhani Singano mwenye kasi na uwezo mzuri wa kutoa krosi kwa fowadi za kati au kumpanga Emanuel Okwi ambaye ni mfungaji na mchezeshaji pia.
Tisa bila shaka ni mchawi wa magoli Hamis Tambwe au anaweza mpaka Kisiga. Maximo ambaye ni mchawi wa saikolojia anaweza kuipanga Yanga katika mfumo ambao utaruhusu viungo wake watawale mchezo na kuziba mianya yote ya Simba kucheza na fomesheni yao( zonal Marking)
Nafasi ya ulinzi Maximo anaweza kuwapanga ; golikipa Deogratius Munish 30, wakati beki namba mbili akisimama Juma Abdul ambaye kadri siku zinavyokwenda amezidi kuimarika na kuitawala vizuri nafasi hiyo.
Mpande wa kushoto ni Oscar Joshua ambaye juzi kwenye mechi na Benin alisimama vizuri kama mlinzi na kuanzisha mashambulizi upande wa kushoto.
Team Capt Nadir ana uhakika kucheza mechi hiyo kama kiongozi na beki tegemeo. Kama kawaida sentafu ni Kelvin Yondani. Anakwenda kucheza mechi hii akiwa na kumbukumbu ya goli zuri alilofunga mechi ya mwisho dhidi ya Ruvu JKT dk ya 34 ya mchezo huo.
Mbuyu Twite ni silaha ya Maximo kama Kiungo mkabaji ambaye pale kati watakutana na Kwizera au Jonas Mkude itategemea Phiri atampanga nani, Winga ya kulia Maximo maximo ana dozen ya wachezaji. Anaweza mpanga Saimoni Msuva , Hassani Dilunga au Said Juma " makapu" .
Wote hao kiasilia ni viungo. Haruna Niyonzima ana uhakika kuanza mechi hiyo kama kiungo mchezeshaji hapo ndipo atakutana aidha na Amri Kiemba au Kwizera lakini mimi naamini hii itakuwa vita kati ya Niyonzima na Kiemba.
Kuna uwezekano mkubwa Hussein Javu akaanza mechi hii na Jaja kusubiri nje ili kuipa kasi timu na kutafuta magoli ya haraka, Mrisho Ngasa akusimama kama kiungo mshambuliaji na Coutinho kucheza winga ya kushoto . Hii ni mechi ya kusisimua sana.
0 comments:
Post a Comment