Azam wamejipanga kutetea ubingwa wao
Na Samuel Samuel
Azam FC mabingwa watetezi wa VodaCom premier League( VPL) wamejipanga hasa kutetea ubingwa wao. Azam ndio timu pekee nchini inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara ambayo angalau inaendeshwa kwa asilimia 60% katika mfumo wa soka la kisasa.
Kuna mambo mengi katika soka la kisasa lakini kwa uchache tu ni kuwa na miundo mbinu mizuri ya soka, uchumi mzuri, waalimu wa kutosha kila idara, hosteli za kisasa na msingi mzuri wa soka la vijana.
Azam katika hayo imegusa kwa asilimia 55% kila sehemu ukilinganisha na timu nyingine za hapa kwetu. Wengi wanajiuliza Azam inaweza kutetea kombe lake mbele ya Yanga, Simba na Mbeya City achilia mbali Mtibwa Sugar ambao msimu huu wanaonekana kujipanga vizuri?
Azam ina nafasi kubwa kutetea ubingwa wake ukitazama vitu vingi kitaalamu na kinadharia. Azam inaundwa na mseto wa wachezaji wenye vipaji tofauti tofauti.
Kuna vijana wenye kiu ya kuchomoza katika soka la Tanzania ( football passion) . Mtazame David Mwantika, Gadiel, Kelvin Friday, Malick, Farid , Mudathir, Aishi Manula na Mao wote hao hawana majina makubwa nchini lakini ndio wanaifanya Azam ikae kileleni mwa ligi.
Ukichukua mseto wa damu hiyo changa ukachanganya na wakongwe kama Boko, Moris, Bolou, Kipre, Mcha, Sure boy , Kavumbagu, Kapombe na Mwaikimba, unapata timu work nzuri kupambana na timu yoyote nchini.
Kinachotoa ishara Azam ipo katika asilimia nyingi za kutetea ubingwa wake ni;
1. Kucheza mechi zaidi ya 30 toka msimu uliopita mpaka sasa bila kupoteza mechi hata moja. Kiufundi hali hiyo inawaongezea hamasa kubwa wachezaji kulinda heshima ya timu na kubaki katika ubora wao.
2. Sera ya mpira ndani ya Azam inatoa mwanya timu hiyo kubaki katika ubora wake. Kocha Joseph Omog amekuwa mjanja sana katika kulinda vipaji vya wachezaji ili asiharibu team work.
Azam naweza sema imesajili wachezaji iwatumie katika ligi na si kusajili tu. Omog analeta ushindani wa namba ndani ya uwanja pia anawapumzisha wachezaji ili kulinda hamu yao ya kucheza.
Mwadini Ali ingawa yupo national team lakini utakuta anawekwa benchi na mlangoni anakaa Aishi Manura.
3. Ujio wa Didier Kavumbagu, Domayo, Diara na Lionel kumeipa nguvu sana timu hiyo katika kushambulia. Ni nani asiyeujua uzuri wa Kavumbagu au Domayo? Hii inaonesha kamati ya usajili ilijipanga kufanya usajili wa maana ili timu itetee kombe.
Domayo bado hajacheza kutokana na majeruhi lakini bado timu ipo vizuri eneo la kiungo cha chini , je akipona itakuwaje?
4. Mwenendo wa Simba na Yanga ambao mara nyungi hupewa nafasi kutwa kombe hilo unawapa nafasi Azam kutetea kombe lake kama hawata tetereka huko mbele ya safari.
Wakati Simba ikicheza mechi nne na kuambulia pointi nne , Azam FC wamecheza nao idadi sawa na kujichukulia Pointi 10. Tayari wamepata ushindi ndani ya uwanja Mgumu wa Soloine na sasa, wamerejea nyumbani Chamazi Dar es Salaam
Kama Azam wataweza kupata pointi mbele ya Yanga , Simba na Mtibwa Sugar, itakuwa imejitengenezea mazingira mazuri kuchukua kombe hilo mara mbili mfululizo.
Mpinzani mkubwa wa Azam FC katika kinyang'anyiro hicho ni Yanga ingawa bado huwezi kumuondoa Simba moja kwa moja. Sasa kama Omog akiweza kuzisoma vizuri mbinu za mbrazili Maximo na Mzambia Phiri, na kupata pointi watakapo kutana, basi Azam FC itazidi kujijengea mazingira mazuri.
0 comments:
Post a Comment