Majembe matatu kutua Old Trafford
Na Oscar Oscar Jr
Manchester United wanatajwa kuendelea kumuwinda kiungo wa Chile na klabu ya Juventus Arturo Vidal na huenda mwezi Januari kwenye dirisha dogo akaweza kujiunga na timu hiyo ya Old Trafford. Bado timu hiyo haijapata dawa ya eneo la kiungo mkabaji na Vidal anatajwa kuwa mwarobaini wa tatizo hilo.
Gazeti la Daily Express wao wameripoti kuwepo mazungumzo kati ya klabu ya Manchester United na beki wa pembeni wa Brazil na timu ya Barcelona, Dani Alves.
Dani anatajwa kutokuwa kwenye mipango ya kocha Luis Enrique na huenda akaondoka kwenye klabu hiyo muda wowote dirisha litakapo funguliwa na United wako mstari wa mbele kumnasa.
Kwa upande wa Sports Witness, wao wamemtaja kiungo mshambuliaji wa Colombia na klabu ya Fiorentina Juan Caudrado kutimka klabuni huko na kujiunga na Man United.
Caudrado alionyesha kiwango bora kwenye michuano ya kombe la dunia kule Brazil na bila shaka ujio wake, utaongeza nguvu kwa Angel Di Maria ambaye anafanya vizuri tangu ajiunge na timu hiyo chini ya Loius Van Gaal.
0 comments:
Post a Comment