Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 October 2014
Thursday, October 23, 2014

Arsenal kusajili beki kwa Pauni Milioni 10.


Na Oscar Oscar Jr

Bada ya timu ya Arsenal kupata ushindi hapo jana wa magoli 2-1 dhidi ya timu ngumu ya Anderlecht kwa magoli ya dakika za mwisho kutoka kwa beki Kieran Gibbs na mshambuliaji Lukas Podolski, kocha wa timu hiyo ameibuka na kutaka kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Arsenal wanajiandaa kumsajili beki wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Leicester City, Liam Moore ambaye amepata kuiwakilisha timu ya U-21 ya Uingereza mara 11 na ni chaguo la kwanza kwenye klabu ya Leicester City inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza. 

Tayari klabu ya Fulham imeshatoa dau la Pauni milion tano na zimekataliwa kwa beki huyo na Arsenal wanaonyesha utayari wa kutoa Milioni 10 zinazohitajika na Leicester City.

Kwa upende wa pili, Arsenal wanaonekana kuzidiwa ujanja na Liverpool katika dili la kumnasa mshambuliaji wa PSG Ezequiel Lavvezi ambaye wamekuwa wakihusishwa naye kwa muda mrefu. 

Liverpool wameibuka na kuonyesha dalili za kumnasa mshambuliaji huyo mwezi Januari baada ya Mario Balotelli kushindwa kuisaidia Liverpool tangu alipojiunga na timu hiyo.

Arsenal walikuwa kwenye mipango ya kumnasa mshambuliaji huyo ili aje kuungana na Danny Welbeck lakini kwa sasa, matumaini yamepotea na Liverpool ndiyo wanaotajwa kuandaa dau la pauni milioni 30 kwa ajili ya Lavvezi ambaye hafurahii maisha ya timu yake ya PSG.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!