Na Chikoti Cico
Mshambuliaji wa Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Christiano Ronaldo akaribia kuivunja rekodi ya mchezaji wa zamani wa Real Madrid Raul Gonzalez ya jumla ya magoli 71 kwenye ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Raul ambaye ameingia mkataba hivi karibuni kuichezea timu ya New York Cosmos alifikisha magoli hayo huku akizichezea timu za Real Madrid na Schalke 04.
Ronaldo aliyefikisha magoli 70 baada ya kufunga goli moja kati ya magoli matatu ambayo Real Madrid iliifunga Liverpool kwenye mchezo wa kundi B wa ligi ya mabingwa Ulaya uliopigwa usiku wa Jumatano uwanjani Anfield, anafukuzana na Messi mwenye magoli 69 kuivunja rekodi hiyo.
Akizungumza baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Liverpool Ronaldo alisema “Sihofii kuhusu hilo, najua ntaivunja rekodi kama sio usiku wa leo basi kwenye mchezo mwingine. pia Messi anaikaribia”
Ronaldo anayeshikilia tuzo ya mchezo bora wa dunia maarufu kama Ballon d'or aliyonyakua mwaka 2013 mbele ya Messi na Ribery, takwimu zinaonyesha mpaka sasa Ronaldo ana magoli 20 kati ya michezo 13 aliyoichezea Real Madrid msimu huu.
Akihojiwa na kituo cha Sky Sport baada ya mchezo dhidi ya Liverpool Ronaldo alisema “Ulikuwa ni mchezo wa timu, tuna alama tisa, asilimia 75 ya kuvuka tayari”
“Ilikuwa ni maalum kwa goli langu la kwanza Anfield na najivunia hilo. Tumepata alama tatu inafurahisha, tulijua kabla ya mchezo kwamba Liverpool wakiwa Anfield ni wagumu lakini tulicheza vizuri hasa dakika 45 za mwanzo na tulistahili kushinda”
0 comments:
Post a Comment