USAJILI LIGI KUU KENYA
Mlinda ngome, Titus Wamalwa na washabulizi Allan Otindo na Geoffrey Simiyu wamejiunga na Kakamega Homeboyz katika pilka pilka zao kuepuka kushushwa daraja katika awamu ya pili ya musimu wa Ligi Kuu Kenya.
Wamalwa na Otindo walitemwa na Karuturi Sport majuzi huku Simiyu akipata hatima sawa kutoka Muhoroni.Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Homeboyz, Cleophas Shimanyula, watatu hao wataongeza ustadi na uzoefu katika kikosi chao.
“Watatu hao tayari wamejiunga nasi. Tulikuwa na haja kubwa ya washambulizi na kuja kwao wenye asili katika Ligi Kuu Otindo na Simiyu kutaongeza matumaini.
“Si siri kwamba Wamalwa ni mlinda ngome mweledi sana na hatutakoma hapo, bado tutaongezea wachezaji wapya pindi tutakapo pata wenye kiwango tunachoazimia,” alinena.
Homeboyz wanashikilia mkia katika Ligi Kuu na wana kibarua kigumu cha kuboresha matokeo kuepuka fedheha ya kushuka ngazi.
0 comments:
Post a Comment