Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 April 2014
Sunday, April 13, 2014

NI HULL CITY VS ARSENAL FAINALI YA KOMBE LA FA



 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Hull City walitoka nyuma mara mbili na kuwatwanga Sheffield United 5-3 kwenye nusufainali ya Kombe la FA iliyochezewa Wembley Jumapili na kufika fainali ya michuano hiyo kwa mara yao ya kwanza kabisa. 

Kwenye kipindi cha kubabaisha cha kwanza, Jose Baxter aliwapa Sheffield United uongozi wa kushangaza dakika ya 19. Yannick Sagbo alisawazishia Hull kunako dakika ya 42, lakini Stefan Scougall akarejesha uongozi wa klabu hiyo ya League One tena kabla ya muda wa mapumziko. 

Hull walipigana kiume kipindi cha pili huku nguvu mpya Matty Fryatt na Tom Huddlestone wakifunga wakifuatana upesi, kabla ya mpira wa kichwa wa Stephen Quinn kuihakikishia klabu hiyo inayocheza Ligi ya Premia ushindi. 

Jamie Murphy aliwafungia United bao la dakika za mwisho la kufutia machozi, kabla ya Hull kuongeza lao la tano kupitia David Meyler. 

Hull sasa watakutana na Arsenal kwenye fainali uwanjani Wembley Mei 17 baada ya timu hiyo ya Arsene Wenger kuwabandua Wigan Athletic kupitia mikwaju ya penalti kwenye nusufainali hiyo nyingine Jumamosi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!