Mchezo baina ya Polis Moro vs Stand United umemalizika.
Na Oscar Oscar Jr
Mkoani Morogoro kulikuwa na mchezo ambao ulizikutanisha timu mbili zilizopanda daraja msimu huu, Polis Morogoro waliwakaribisha Stand United kwenye mchezo wa mzunguko wa tisa na matokeo ya mchezo huo ni timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya 0-0.
Stand United ambao kuelekea mchezo huo walikuwa wametoka sare ya wakongwe kama Simba, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, wamejikuta wakipata pigo kwa mchezaji wao wa kutumainiwa Harouna Chanongo kuonyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya wamalize pungufu.
Matokeo hayo yamewafanya Stand kutimiza pointi 11 huku Polis Morogoro wakifikisha alama 13 baada ya kujikusanyia alama nne kwenye mechi mbili za hivi karibuni wakicheza kwenye uwanja wa nyumbani wa Jamhuri Morogoro.
Polis Morogoro sasa wanajiandaa kwenda kucheza na timu ya Ndanda kule mkoani Mtwara na kisha watasafiri kuelekea mkoani Tanga ambako watakwenda kucheza na Coastal Union kwenye dimba la Mkwakwani.
Baada ya kucheza mechi mbili mfululizo, Stand United bado wataendelea kubaki ugenini na sasa ni zamu ya kwenda kuwavaa Ruvu JKT kwenye uwanja Azam Complex na kisha, watarejea nyumbani kuwaalika Azam fc.
0 comments:
Post a Comment