Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 April 2014
Saturday, April 12, 2014

MSHAMBULIAJI BENTEKE SASA KUFANYIWA UPASUAJI



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Straika wa Aston Villa Christian Benteke atafanyiwa upasuaji nchini Ubelgiji kufuatia jeraha la kano za kisigino ambalo lilitibua ndoto yake ya kucheza Kombe la Dunia. 

Benteke alijeruhiwa akifanya mazoezi Alhamisi iliyopita na meneja wa Villa Paul Lambert Alhamisi alithibitisha kwamba mchezaji huyo sasa amerudi nchi alimozaliwa kufanyiwa upasuaji. 

“Daktari wetu (Roddy Macdonald) yuko Ubelgiji na amewasiliana na daktari wa upasuaji, na kuna uwezekano kwamba atafanyiwa upasuaji – leo, usiku au kesho,” Lambert akasema. 

“Baada ya hapo, yote yatakuwa kuhusu kupona kwake. Ukiwa na jeraha la muda mrefu, huwa una siku njema na siku mbaya wakati mmwingine, kama mtu mwingine yeyote aliye na jeraha linalomuweka nje muda mrefu, lakini atakuwa sawa.”

Ingawa Benteke, 23, hatacheza Kombe la Dunia nchini Brazil na huenda asicheze hadi Oktoba, Lambert ana imani kwamba hatakufa moyo na kwamba atajizatiti kurudi mchezoni mapema iwezekanavyo. 

“Lakini kwa sasa ndio ukweli unamfikia kwamba atakosa Kombe la Dunia, ambalo ni pigo kuu,” Lambert akaongeza.
“Lakini yeye yuko kwenye kizazi cha wachezaji wa Ubelgiji ambao watacheza dimba kadha miaka ijayo. 

“Bado ni mchanga katika kundi hilo, na atarudi akiwa na nguvu zaidi, ukizingatia alivyo na mwili wake.
“Bila shaka, kila mtu ni tofauti kuambatana na anavyopiga hatua, na vile mwili hupona. 
"Lakini ukiangalia Christian na vile alivyo, atafanya vyema na kujizatiti kurudi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!