Na Chikoti Cico
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alalamikia msongamano wa ratiba kati ya ligi kuu ya Uingereza na Capital one cup, Chelsea ambao wamelazimika kusafiri baada ya masaa 48 toka walipocheza mchezo wa ligi dhidi ya Manchester United mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford na kuisha kwa matokeo ya sare ya goli 1-1 kwaajili ya kujiandaa na mchezo wa Capita one Cup dhidi ya Shrewsbury.
Chelsea ambao mpaka sasa wanaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza huku wakiwa na alama 23 walisafiri umbali wa maili 170 kwa basi kuelekea kenye mechi hiyo dhidi ya Shrewsbury inayocheza ligi daraja la pili, mchezo huo utapigwa kwenye uwanja Greenhous Meadow siku ya Jumanne.
Jose Mourinho akioneshwa kukerwa na msongamano huo wa ratiba alisema “Tupo matatizoni kwasababu tuna wachezaji wengi majeruhi na hiyo inafanya ugumu zaidi kwetu, tuna siku moja ya kujiandaa.” Aliendea kusema “Tuna mechi ngumu kwasababu wanafanya vizuri kwenye ligi yao na wanafanya vizuri dhidi ya timu kubwa kwenye Capital One Cup.
Ni siku kubwa kwao, tunajua itakuwa siku ngumu kwetu ila huo ni mpira”
Akiendelea kuongelea mchezo huo Mourinho alisema “Shrewsbury ni Capital One Cup na sio mechi ya kirafiki, inatuhitaji tucheze kwa heshima na njia nzuri ya kuiheshimu Shrewsbury kwenye Capital One Cup ni kwenda pale na timu bora na sio kwenda na timu na dhaifu.
Kama wakishinda washinde dhidi ya timu bora, tuna hali mbaya ila ukiangalia wachezaji ambao hawakucheza, Schurrle, Salah, Zouma, Ake, Mikel hawa vijana ni wazi watacheza”.
Wakati huo mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ambaye alikuwa majeruhi na kushindwa kucheza kwenye mechi tatu zilizopita dhidi ya Crystal Palace, Maribor na Manchester United anatarajiwa kurejea uwanjani siku ya Jumamosi wakati Chelsea itakapokuwa inacheza dhidi ya QPR.
0 comments:
Post a Comment