Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 October 2014
Thursday, October 23, 2014

Hawa ndiyo maadui wa Yanga


Na Mwandishi wetu

Yanga SC ina nafasi kubwa sana kurudisha heshima yake katika soka la Tanzania bara. Tayari wababe hao wa Jangwani wameonesha nia ya kurudi kileleni kwenye soka la Tanzania panapotawaliwa na wana lamba lamba toka pale Chamazi. 

Yanga inayonolewa na Mbrazil Maximo " the chose one" itashindwa kufikia malengo hayo kama mambo yafuatayo hayatarekebishwa mapema; 

1. Kuna baadhi ya wanachama na viongozi wa zamani wa Dar Young African wamekuwa hawaukubali uongozi uliopo madarakani. Hali hii imeua umoja na mshikamano wa dhati wa klabu hii kongwe nchini. Wengi wanahoji kitendo cha Mwenyekiti kuongezewa muda wa kukas madarakani. 

Hali hii inawavunja moyo viongozi waliopo madarakani na kujikuta hawaitumikii klabu yao kwa 100%. Ifike wakati wanachama waheshimu maazimio ya mkutano mkuu ili viongozi waungane katika umoja wao kuitumikia klabu yao. Utawala ukitulia klabu itafika mbali maana itapata kila kitu kwa wakati . 

2. Kuingiliwa kwa benchi la ufundi. Kuna kila dalili ya Maximo kuwa katika msongo mkubwa wa mawazo kwa sasa kwa kukosa ushindi kwenye mechi ya Mtibwa Sugar na Simba SC. Tayari wenye nyoyo nyepesi wameanza kuhoji uwezo wa mwalimu huyo. 

Kitendo cha kuliweka benchi la ufundi kikaangoni ni kupunguza ufanisi wao. Mashabiki wa Yanga , viongozi na wanachama wanapaswa kufahamu kuwa, Yanga ni timu kama timu nyingine zinazohitaji ushindi na mpira una matokeo ya aina tatu. Kushinda, kufungwa au kudroo. Mbali na hayo Maximo bado yupo vizuri na timu yake. 

 Amekusanya pointi saba katika mechi nne akitanguliwa na Mtibwa Sugar na Azam Fc wote wapo kileleni wakiwa na pointi kumi. Hivyo benchi la ufundi linahitaji uhuru zaidi. 

3. Kingine ambacho ni kikubwa sana, Maximo bada hajafanikiwa sana kuisoma falsafa ya soka la Tanzania. Bado amejichimbia katika mzizi ya soka la kwao Brazil. Soka la Tanzania limejaa vitimbwi vya kila aina. Watanzania bado tuna amini katika fitina chafu ili tupate matokeo mazuri. Ni lazima kama meneja wa timu asikubali fikra za kuhujumiwa timu ziingie kichwani mwake wala kwa wachezaji wake.

Tayari fununu za hujuma zimeanza kuingia kwenye klabu hiyo. Hiyo inatokana na habari ambazo sio rasmi  zilizo zagaa kwamba watu hawa mtaki kocha huyo na uongozi uliopo madarakani. 

4. Adui mwingine ni mwalimu mwenyewe. Inasadikika Maximo ni mgumu sana kushaurika. Mifumo anayotumia na baadhi ya wachezaji anao watumia , atachelewa sana kupata matokeo mazuri kama ilivyokuwa kwa babu Hans. 

Mbali na uwezo wa mchezaji kama Jaja kutiliwa mashaka, lakini Maximo amekuwa akiendelea kumtumia mchezaji huyo. Kuwaweka nje wachezaji wenye kasi na ufahamu mkubwa wa ligi ya nyumbani kama , Kiiza, Javu, Tegete , Bahanuzi na Hamisi Thabiti mwisho wa siku kutaigawa timu katika matabaka. 

Hatuwezi ingilia mfumo wa mwalimu lakini inampasa kutoa nafasi kwa wachezaji wengine. Kuna mambo mengi sana lakini hayo yakifanyiwa kazi , Yanga itarudisha heshima yake.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!