Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 October 2014
Friday, October 17, 2014

Didier Kavumbagu dhidi ya Mbeya City.



 Na Samuel Samuel

Wakati Mbeya City wakijivunia mchezaji bora wa mwezi Septemba Antony Matongolo kama ilivyotanabaishwa na wadhamini wa ligi " VODACOM", Azam FC wana mshambuliaji wa kati hatari zaidi nchini kwa sasa. Huyu si mwingine bali ni Mrundi Didier Kavumbagu. 

Mpaka sasa kwenye ligi kuu Tanzania bara ndiye mshambuliaji anaeongoza kwa ufungaji wa mabao baada ya kujikusanyia kibindoni magoli manne(4). 

Beki ya Mbeya City inahitaji kumchunga zaidi mchezaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kujiweka kwenye njia nzuri ya kutupia magoli. 

Didier Kavumbagu akiwa Dar Young Africans, kocha Brandts na hata Hans Van Pluijm walikuwa wanamtumia kama super sub kutokana na uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo na kubadilisha matokeo. Kama unakumbuka mechi kati ya Yanga na Oljoro JKT msimu uliopita mpaka timu zina kwenda mapumziko ilikuwa ni 0-0.

Lakini kipindi cha pili alipoingia, aliubadiri mchezo. Aliingia kama play maker dakika ya 72 ya mchezo na dakika mbili baadae, Yanga wakapata magoli kupitia kwa Zahir na Ngasa kazi kubwa ikifanywa na yeye. 

Kiasilia Kavumbagu ni kiungo mshambuliaji. Ana uwezo mzuri kucheza kama mshambuliaji wa kati au namba kumi. Mbeya City wasipokuwa makini, krosi zote zitakazokuwa zinachongwa toka upande wa kulia au kushoto, kavumbagu ni mmaliziaji mzuri. 

Kocha Omog kuna uwezekano akamuanzisha Didier na Gaudance Mwaikimba kwenye safu ya ushambuliaji huku, Kavumbagu akicheza kama namba 10.

 Mwaikimba anaonekana kama yupo taratibu lakini, kama Salum Abubakary ataanza kama kiungo mchezeshaji, anaweza kumlisha mipira Mwaikimba kwa sababu kasi yao inaendana na kuiangamiza Mbeya City.

Winga ya kulia akimpanga Himid Mao na kushoto akimwacha Kipre Tchetche, hapo Didier atakuwa amezungukwa na watu makini wa kumtengenezea nafasi nzuri ya kuibomoa ngome imara ya Mbeya City inayoundwa na kina David Buruhani, Kaseke , Mazanda na wengineo. 

Mwambusi ana kazi ya ziada kumzuia mnyama huyu. Kavumbagu amebarikiwa vitu vingi , kasi, uwezo wa kumiliki mpira na mbinu mbadala ya kuisoma ngome ya adui. Kikubwa ni uwezo wa kufunga katika mazingira magumu. 

Mechi kati ya Azam Fc na Polisi Moro, alifunga magoli mawili katika mazingira magumu sana. Polisi Moro ingawa ilipoteza mchezo ule lakini bado ilikuwa na beki imara. Hivyo basi kesho itakuwa ni kazi kubwa kati ya viungo na walinzi wa Mbeya City kumzuia Kavumbagu. 

Ikumbukwe Kavumbagu alimaliza msimu uliopita akiwa na magoli 11 akiwa na klabu ya Yanga lakini, msimu huu katika mechi tatu tu ana magoli manne ! Hiyo ni salamu kwa Mwambusi kesho.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!