Debuchy nje miezi miwili.
Na Chicoti (Cico cicod)
0755 700 076
Timu ya Arsenal yaendelea kukumbwa na majeruhi baada ya beki wake wa kulia Mathieu Debuchy kuumia kifundo cha mguu kwenye mechi ya ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester City iliyopigwa kwenye uwanja wa Emirates na kuisha kwa sare ya 2-2.
Debuchy aliyejiunga na Arsenal akitokea timu ya Newcastle United anategemewa kuwa nje kwa muda wa miezi miwili baada ya kuumia kifundo cha mguu, kutokuwepo kwa Debuchy kutamlazimisha kocha Arsenal Wenger kumpanga beki wa katikati Calum Chambers kama beki wa kulia mpaka Debuchy atakaporejea uwanjani.
Arsenal itamkosa Debuchy kwa mechi kadhaa za ligi ya Uingereza dhidi ya watani wao Tottenham na pia dhidi ya Chelsea, lakini pia itamkosa kwa mechi kadhaa za ligi ya mabingwa Ulaya, Arsenal wanatarajiwa kufungua pazia la michuano ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Borussia Dortmund siku ya Jumanne.
Baada ya kumuuza Bacary Sagna kwa timu ya Manchester City na kumsajili Debuchy kama mbadala wake kunafanya kuumia kwa beki huyo wa kulia kuwa pigo kwa sehemu ya ulinzi ya Arsenal.
0 comments:
Post a Comment