Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 September 2014
Monday, September 15, 2014

Rooney afikia rekodi ya Henry.



Na Chicoti (Cico cicod)
 0755 700 076


Nahodha wa Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney afikisha magoli 175 kwenye ligi kuu ya Uingereza akifikia rekodi kama hiyo hiyo iliyowekwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ambaye kwasasa anakipiga kwenye timu ya Ney York Red Bulls katika ligi kuu ya Marekani maarufu kama “ Major League Soccer”. 

Wayne Rooney aliweza kufikia rekodi ya Henry kwa kufikisha goli la 175 baada ya kufunga goli la tatu la Manchester United katika mechi dhidi ya QPR, mechi ambayo iliisha kwa United kushinda kwa magoli 4-0 ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha mpya wa Manchester Luis Van Gaal kwenye ligi kuu ya Uingereza. 

Kwa pamoja Henry na Rooney wanashika nafasi ya tatu kwenye listi ya wafungaji bora wa muda wote kwenye ligi kuu ya Uingereza wakiwa nyuma ya Andre Cole anayeshika nafasi ya pili akiwa na magoli 187 na Alan Shearer anayeshika nafasi ya kwanza akiwa na magoli 260. 

Katika umri wa miaka 28 imemchukua Wayne Rooney michezo 377 kuweza kufikia rekodi ya magoli 175 kwenye ligi kuu ya Uingereza sawa na Henry ambaye kipindi akiichezea Arsenal ilimchukua michezo 258 kuweka rekodi hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!