Man United wampa zawadi mke wa Van Gaal.
Na Chicoti (Cico cicod)
0755 700 076
Manchester United hatimaye wapata ushindi wao wa kwanza kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga timu ya QPR kwa magoli 4-0, QPR inayofundishwa na kocha Harry Redknapp ilionekana kutokuleta upinzani mkali kwa United.
Iliwachukua dakika 24 toka kuanza kwa mechi kwa Manchester United kuandika bao la kwanza kupitia kwa Angel Di Maria kwa mpira wa adhabu ndogo ulioenda moja kwa moja wavuni.
Ander Herrera aliweza kuipatia United goli la pili kwa shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni baada ya kupokea pasi kutoka kwa Wayne Rooney .
Ikiwa imebaki dakika moja kwenda mapumziko Rooney aliipatia United goli la pili baada ya kugongeana vyema na Herrera, hivyo hadi mapumziko walikuwa ni Manchester waliotoka kifua mbele dhidi ya QPR kwa kuongoza kwa magoli 3 kwa bila.
Dakika ya 58 Juan Mata alihitimisha ushindi wa mashetani wekundu baada ya kufunga goli la nne akitumia makosa ya ngome ya ulinzi ya QPR iliyokuwa chini ya beki wa zamani wa Manchester United mwingereza Rio Ferdinand.
Pia ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa wachezaji wapya waliosajiliwa na United kucheza hasa Rojo, Blind na Falcao aliyeingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Juan Mata.
Kocha wa Manchester United aliutoa ushindi huo kama zawadi ya siku ya kuzaliwa kwa mkewe Truus akiwa mwenye furaha akihojiwa na waandishi wa habari baada ya mchezo huo alisema “ Hii ni maalumu kwasababu pia ni siku ya kuzaliwa mke wangu, mke wangu alisema zawadi kubwa iwe ni ushindi na tumempa” .
0 comments:
Post a Comment