Real Madrid yaibuka kidedea
Na Oscar Oscar Jr
Real Madrid jana usiku ilishusha mastaa wake kadhaa waliosajiliwa msimu huu kwenye mechi ya kwanza ya La Liga ndani ya Santiago Bernabeu na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cordoba timu iliyopanda daraja.
Mabao ya mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema na nyota mkubwa wa Ureno, Cristiano Ronaldo, yalifanikiwa kuzima upinzani wa hali ya juu kutoka timu ya Cordoba ambao wamepanda daraja kucheza La Liga musimu huu.
Pamoja na ushindi walioupata Real Madrid bado hawakuonyesha mchezo mzuri. Toni Kros, James Rodriquez hawakuonekana kufanya vema huku Christiano Ronaldo akionekana kukasirika kila alipokabwa na mwamuzi kumpotezea.
Bado Real Madrid haina mshambuliaji mwingine wa kusaidizana na Benzema huku Alvaro Morata akielekea Juventus na kiungo mshambuliaji Angel Di Maria, ameondoka na kujiunga na Manchester United.
Kuondoka kwa Dimaria kumuonyesha pengo kwani walionekana kukosa mtu sahihi wa kutengeneza nafasi za kufunga.
0 comments:
Post a Comment