Man United yaendelea kumwaga noti
Na Chicoti (Cico cicod)
0755 700 076
Klabu ya Manchester United tayari imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Angel Di Maria akitokea klabu ya Real Madrid na sasa atakuja kuungana na Juan Mata, Ander Herrera, Marcos Rojo na Luke Shaw ambao watatakiwa kuokoa jahazi la timu hiyo linaloendelea kuzama.
Baada ya kufanya usajili wa beki wa kushoto Marcos Rojo kutoka Sporting Lisbon kwa ada ya paundi milioni 16, timu ya Manchester United imekamilisha usajili wa Angel di Maria kutoka Real Madrid kwa ada inayoweza kufikia paundi milioni 60 huku akipewa mkataba wa miaka mitano kwa mshahara unaoweza kufikia paundi laki mbili kwa wiki.
Huku kipindi cha usajili kikikaribia kuisha United wanajitahidi kukiongezea makali kikosi cha Luis Van Gaal, huku mtendaji mkuu wa Manchester Ed Woodward akijitahidi kutafuta sahihi za wachezaji mbali mbali watakaofiti kwenye mfumo wa kocha mpya baada ya kuanza ligi kwa kusua sua.
Katika umri wa miaka 26 Di Maria atakuwa mchezaji wa pili United kuingiza kipato kikubwa, hii ni kwa kupokea mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki akizidiwa na nahodha Wayne Rooney peke yake anaepokea kitita cha paundi laki tatu kwa wiki.
Di Maria anajiandaa kuungana na wachezaji wengine wa Manchester United kwa mazoezi ya kujiandaa na mechi ya Jumamosi dhidi ya Burnley katika mbio za kocha Luis Van Gaal kutafuta ushindi wake wa kwanza kwenye ligi kuu ya Unigereza.
0 comments:
Post a Comment