Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 April 2014
Monday, April 21, 2014

UJIO MPYA WA JACK WILSHERE



 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere atakuwa sawa kucheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Hull City mwezi ujao na “atakuwa amenolewa” vya kutosha kuwa katika kikosi cha Uingereza kitakachocheza Kombe la Dunia, meneja Arsene Wenger amesema.
Wilshere hajacheza tangu apate jeraha la mfupa wa mguu akichezea Uingereza chini ya Roy Hodgson wakati wa ushindi wao wa 1-0 mechi ya kirafiki dhidi ya Denmark uwanjani Wembley mwezi Machi. 

"Ataanza kukimbia polepole wiki hii. Ninafikiri atakuwa sawa katika wiki mbili au tatu,” Wenger alinukuliwa na vyombo vya habari vya Uingereza Jumapili. 

"Nilinena na Roy Hodgson na nikamwambia Wilshere ataweza kuchezea Uingereza. Atakuwa amenolewa vyema kuchezea Uingereza. Jack anaweza kuwa wa kushangaza."
Jeraha hilo lilikuwa la karibuni zaidi kutatiza kiungo huyo wa miaka 22, aliyechezea Arsenal mechi yake ya kwanza akiwa na miaka 16 Septemba 2008. 

Alikosa msimu wote wa 2011-12 na Euro 2012 baada ya kujeruhiwa kifundo cha mguu wakati wa mechi ya kirafiki ya kabla ya msimu. 

Wenger alisema aliyopitia mchezaji huyo wakati wa mejaraha hayo huenda yakamfaa mwishowe.
"Ndilo jambo ngumu zaidi kukabiliana nalo. Lazima uwe na ushindani, ambao hutokana na kushiriki mashindano kila wakati,” alisema Mfaransa huyo. 

"Jack amekuwa ndani na nje mwaka huu, lakini nafikiri sasa wamemaliza tatizo. Ninafikiri kutoka sasa kwenda mbele ataweza kucheza. Jack ni mtu wa kucheza soka. Ni wale ambao ukiwaambia kitu, ana ufahamu asilia wa soka. 

"Huwa anaangalia mechi na kutathmini vyema yale yanayoendelea,na upande huo amaejifunza mengi akiwa amejeruhiwa, kwa kutazama mechi na kujua matatizo ambayo anaweza kukabiliana nayo wakati wa mechi.”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!