Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 April 2014
Friday, April 11, 2014

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YATAMBULISHWA BUNGENI


Na Boniface Wambura


Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania iliyotwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani nchini Brazil baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 kwenye fainali imetambulishwa leo (Aprili 11 mwaka huu) katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma. 


Baadaye timu hiyo leo itapata chakula cha mchana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda. Saa 10 jioni itatembeza kombe hilo katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma katika gari za wazi. 

Jioni imeandaliwa hafla maalumu ya chakula pamoja na burudani hapo hapo mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara. 

MWENYEKITI WA CECAFA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI 

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga atakuwa na mkutano na waandishi wa habari Jumatatu (Aprili 14 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizopo Ghorofa ya 3, Jengo la PPF Tower mtaa wa Ohio/Garden Avenue kuanzia saa 5 kamili asubuhi. 

BONIFACE WAMBURA OFISA HABARI NA MAWASILIANO SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!