Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 April 2014
Sunday, April 06, 2014

LIVERPOOL HAWAKAMATIKI MBIO ZA EPL




Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Liverpool waliendeleza juhudi zao za kutwaa ubingwa wa Ligi ya Premier ya Uingereza baada ya nahodha Steven Gerrard kutingisha penalti iliyokamilisha ushindi wa 2-1 dhidi ya West Ham Jumapili. 

Refa Anthony Taylor alichangia pakubwa ushindi huo baada ya kuashiria penalti ambayo ilioneka bandia baada ya kukubali bao la kusawazisha kwa vijana wa nyumbani, West Ham, ingawa kipa wa Liverpool, Simon Mignolet, alikuwa ametendewa makosa yalioonekana wazi. 

Gerrard alifunga la kwanza na mkwaju wa penalti katika kipindi cha kwanza ambayo ilikuwa halali na bao lake la pili kupitia njia hiyo liliinua kapteni huyo hadi nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora kwenye historia ya timu yake nyuma ya Kenny Dalglish. 

Washindi hao sasa wamo alama mbili mbele ya  Chelsea na nne mble ya Manchester City walio nafasi ya tatu huku Liverpool,wakialika City ambao wana mechi mbili ya ziada wiki ijayo dimbani Anfield. 

“Kulikuwa na maamuzi mabaya dhidi yetu na wao lakini hakuna ubishi tulikuwa timu bora zaidi.
“Kusema ukweli, refa alikuja kwetu na kukiri alifanya makosa kupitia bao lao la kusawazisha lakini pangu, kulikuwa na uwezekano wa kupatiana penalti ya pili,” kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers, alisema baada ya mechi hiyo. 

Ingawa mjadala mkubwa utazingira waamuzi, kurunzi ilielekezewa Liverpool kabla ya mechi huku washambuliaji wao matata, Luis Suarez na Daniel Sturridge, wakimulikwa kwasababu ya umaahiri wao mbele ya lango. 

Suarez alikosa nafasi bora dakika ya tatu na 16 baada ya mvutano huo kuanza lakini viungo wa Rodgers walisitiri utulivu na kuchukua uongozi ikisalia dakika moja kabla ya kipindi cha mwanzo kuanza. 

Bila kumung'unya maneno, Suarez alibuni fursa ya kufunga pale aliposambaratisha ngome ya West Ham na kufikia pasi ya Gerrard na alipomvisha James Tomkins kanzu, beki huyo aliunawa kwenye mkono na nahodha wake akapachika wavuni. 

Uongozi huo ulidumu muda mchache kwani katika muda wa ziada wa kipindi hicho, straika wa zamani wa Liverpool, Andy Caroll, aliruka kuvamia kona lakini alimgonga Mignolet kichwani na kipa huyo aliachiria mpira kwa guu la Demel aliyefunga kutoka hatua chache. 

Liverpool walilalamika bila mafanikio kuwa kipa wao alichezewa visivyo huku Suarez akimwonesha Taylor marudio katika runinga lakini refa huyo hakutikisika na alikubali bao hilo kufuatia uamuzi wa msaidizi wake Stuart Burt aliashiria kwa kibendera kwamba juhudi hiyo ilikuwa halali. 

Lakini waliweza kutamba pale Taylor alipoamua kuwa kipa wa West Ham, Adrian, alimwangusha mlinda ngome wa Liverpool, Jon Flanagan, kwenye eneo la hatari licha ya kuwa alipata mpira kabla ya mchezaji na Gerrard alikubali jukumu la kutinga la pili bila tashwishi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!