Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 April 2014
Sunday, April 06, 2014

ARSENAL WACHEZEA VITASA MBELE YA EVERTON



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Everton walijiongezea matumaini yao ya kufuzu kombe la mabingwa pale waliposongea hadi alama moja pekee nyuma ya Arsenal wanaomiliki nafasi ya nne kupitia ushindi wa 3-0 dhidi ya timu hiyo Jumapili nyumbani kwao Goodison Park.

Magoli kutoka Steven Naismith, Romelu Lukaku na bao la kujifunga mwenyewe kutoka mchezaji wao wa zamani, Mikel Arteta, yaliongoza Everton kuwatoa Arsenal manyoya kwa njia ya ufarsafa. 

“Tulicheza mchezo mzuri na la kunogesha zaidi ni jinsi ngome yetu ilivyomudu mashambulizi yao na nidhamu tulipokosa mpira,” meneja Roberto Martinez, alisema baada ya ushindi huo. 

Mwenzake Arsene Wenger aliyehuzunika alikiri kuwa vijana wake walikosa kupigania alama tatu na kuchakazwa kwao kulizua wasi wasi mkubwa miongoni mwa wachezaji wa miamba hao wa kutoka kastakizi mwa London. 

“Hatuna budi kuchuguza yaliotokea na kurudi tukiwa na ari tofauti ili kumudu changamoto zijazo. Ni lazima turejelee kwenye msingi,” aliongezea wenger. 

Naysmith alifungua magoli dakika ya 14 pale kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, alipozuia kombora la Lukaku na miguu kabla ya viungo wa Martinez kupanua mwanya dakika 20 baadaye pale Lukaku alipotia kimyani goli la kusisimua baada ya kuichenga ngome ya wapinzani wao na kuachilia kombora kali. 

Arsenal walianza kipindi cha pili na kuvizia wenyeji wao ili kuokoa jahazi lakini walizimwa dakika ya 62 pale Kevin Mirallas alipompokonya Bacary Sagna boli na kumuunganishia Naysmith lakini baada ya Szczesny kuokoa, Mirallas na Arteta walipigania mpira lakini mchezaji huyo wa Arsenal alifanikiwa kuelekeza langoni mwao na kufunga udhia.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!