Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 April 2014
Sunday, April 06, 2014

BAYERN YAPIGWA "FULL STOP"



 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Augsburg waliwapiga "full stop" mbio zao za bila kufungwa timu ya Bayern Munich ambapo walikuwa wamefikisha idadi ya mechi  53 za ligi, ambayo ni rekodi, kwa kuwatwanga 1-0 kwenye Bundesliga Jumamosi wiki hii. 

Kocha wa Bayern Pep Guardiola alipumzisha wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Jumatano dhidi ya Manchester United. 

Augsburg ambao ni majirani wa Bayern Munich maarufa kama "The Bavarians" walitumia vyema mabadiliko hayo, kwa kufunga bao la ushindi kipindi cha kwanza kupitia kwa Sascha Moelders baada ya Mitchell Weiser aliyekuwa akichezea Bayern mara ya kwanza kupokonywa mpira na Daniel Baier. 

Na kule chini, VfB Stuttgart walilaza Freiburg 2-0 na kuondoka kutoka kwa timu tatu za mwisho, huku Nuremberg wakishuka hadi nambari ya pili kutoka mwisho baada ya kupokezwa kichapo cha 2-0 nyumbani dhidi ya Borussia Moenchengladbach, ambao wamepanda hadi namabri nne. 

Kwingineko, Schalke walisalia nambari tatu baada ya kutoka sare 1-1 wakiwa Werder Bremen, nao Eintracht Frankfurt wakawacharaza majirani zao Mainz kwa bao 2-0.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!