Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 April 2014
Saturday, April 05, 2014

MAN UNITED HATIMAYE GARI LIMEWAKA



 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Mabao mawili makali muda mfupi kabla ya muda wa mapumziko yalisaidia Manchester City kuiponda Southampton 4-1 Jumamosi na kuzidisha presha kileleni mwa Ligi ya Premia.

Penalti iliyopigwa na Rickie Lambert ilikuwa imefuta bao la mapema la Yaya Toure ambalo pia lilitokana na penalty, lakini makombora makali ya Samir Nasri na Edin Dzeko yakawaweka mabingwa hao wa 2012 mbele 3-1 kabla ya mapumziko, nafuu ambayo walizidisha kupitia Stevan Jovetic dakika sita kabla ya mechi kuisha. 

City walipanda hadi nambari mbili wakiwa na alama 70, moja nyuma ya Liverpool ambao watacheza dhidi ya West Ham United Jumapili. 
 City wana mechi moja ambayo hawajacheza wakilinganishwa na wapinzani wao keleni. Matokeo hayo yalikuwa makali kiasi kwa Southampton walio nambari nane na ambao walikuwa wanatishia kabla ya kufungwa mabao hayo mawili ya kasi, muda mfupi baada ya mfungaji mabao bora wao Jay Rodriguez kuanguka vibaya, na kuondolewa uwanjani kwa machela na kutilia shaka matumaini yake ya kutajwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakachocheza Kombe la Dunia.

Manchester United nao walipanda hadi nambari sita kwa ushindi mkubwa wa 4-0 ugenini Newcastle United, Juan Mata akiwafungia mawili na Javier Hernandez na Adnan Januzaj wakaongeza moja kila mmoja. 

Fulham nao waliondoka kwenye mkia wa jedwali kwa ushindi wa 2-1 wakiwa Aston Villa.
Bao la ajabu la Kieran Richardson lilifutwa na Grant Holt, kabla ya Hugo Rodallega kuwatwalia alama hizo tatu muhimu na kuwezesha Fulham kutumia vyema kushindwa kwa Cardiff 3-0 nyumbani dhidi ya Crystal Palace. 

Mabao mawili ya Jason Puncheon na moja la Joe Ledley yaliendeleza msururu mbaya wa matokeo upande wa Cardiff chini ya Ole Gunnar Solskjaer. Fulham sasa wamesonga juu ya Cardiff na Sunderland wakiwa na alama 27. 

Cardiff wamo nambari 19 na alama 26 huku Sunderland, ambao watacheza na Tottenham Hotspur Jumatatu wakiwa alama moja nyuma, lakini wakiwa na mechi tatu ambazo hawajacheza. 

West Bromwich Albion, ambao hatimaye wanaonekana kugundua ustadi wao tena chini ya Pepe Mel, waliwalaza Norwich City 1-0 nalo bao la George Boyd likawapa Hull City ushindi wa 1-0 dhidi ya Swansea City.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!