Mlinda mlango wa Barcelona na timu ya taifa ya
uhispania, Victor Valdes hatashiriki fainali za Kombe la dunia baada
ya kupata jeraha kwenye mshipa wa mguu.
Victor mwenye umri wa miaka 32 aliondolewa
uwanjani kwa machela wakati wa mechi kati ya Barcelona na Celta Vigo,
ambapo Barcelona iliinyuka timu hiyo magoli 3-0 siku ya jumatano.
Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa mchezaji huyo amepata jeraha na kuwa atahitaji kufanyiwa upasuaji.
Inaelezwa kuwa kutokana na hali hii huenda
Valdes ukawa ndio mchezo wake wa mwisho akiwa na Barcelona na ataondoka
kwenye klabu hiyo mkataba wake utakapomalizika kipindi cha majira ya
joto.
Kocha wa Barcelona, Gerardo Martino amesema
hakuna mpango wa kumtafuta mlinda mlango mwingine na kuwa atamaliza
msimu huu na kikosi alichonacho.
Victor alipata jeraha dakika ya 22 katika dimba
hilo lililokuwa Nou Camp, muda mfupi baada ya kupangua mpira wa adhabu
wa Celta Vigo.
Valdes, ambaye ambaye ameichezea Barcelona kwa
miaka 12, alikuwa akitegemewa kupambana na Iker Casillas kupata nafasi
ya kuidakia timu ya taifa ya Uhispania katika michuano ya kombe la dunia
nchini Brazil mwaka huu lakini fursa hiyo imeonekana kuwa finyu kwake.
Valdes amepata jeraha ikiwa ni mara ya pili
katika msimu huu mara ya kwanza alipata jeraha kwenye kifundo cha mguu
wakati Uhispania ilipocheza mechi ya kirafiki na Afrika kusini mwezi
Novemba
mwaka jana na kufungwa 1-0.
Jeraha hilo lilimfanya Valdes kukosa mechi nane ya Barcelona.
0 comments:
Post a Comment