Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri sare ya 2-2 dhidi ya Swansea
City inatishia uwezo wao wa kumaliza miongoni mwa nne bora katika ligi
ya Premier ambayo inachacha moto.
Ndoto yao ya kulinyakua taji hilo kwa mara ya kwanza tangu 2004
ilididimia baada ya sare hiyo ya nyumbani huku wakibaki alama sita nyuma
ya viongozi Chelsea.
Arsenal wana kibarua kikali katika mechi zao mbili zinazofuatia
kwani watakung'utana na Manchester City walio mbele na Everton walio
nyuma yao katika jadwali.
Everton waliicharaza Newcastle 3-0 na kusonga alama sita nyuma ya Arsenal huku wakiwa na mechi moja ya ziada.
“Kwa sasa, kushinda taji sio lengo letu kuu kwani hatuna budi ili kukubali yanayojili.
“Kwa sasa, inaonekana hakuna yeyote mwenye uwezo wa kuzuia City
kwani wana mechi mbili za ziada na sasa, inabidi tutizame nyuma yetu
kwani Everton wanakaribia,” Wenger alisema.
“Sare yetu ilivunja moyo lakini ni lazima tujitayarishe vilivyo kwa mechi inayofuata,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment