Everton waliimarisha matumaini yao ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kuilaza Newcastle 3-0 Jumanne, kwenye ushindi wa kupendeza ambao ulianzishwa na bao maridadi kutoka kwa Ross Barkley.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alichomoka kutoka nusu yao ya uwanja na kuwasambazaa walinzi wa Newcastle kabla ya kutoa kombora kali dakika ya 22.
Romelu Lukaku alifunga dakika ya 52 kabla ya Leon
Osman kukamilisha ushindi wao kwa bao la tatu dakika ya 87 baada ya bidii za Gerard Deulofeu, aliyeandaa mabao yote matatu.
Everton wako alama sita nyuma ya Arsenal walio nambari nne wakiwa na mechi moja ambayo hawajacheza.
0 comments:
Post a Comment