Na Hafidhi Kido.
Zimezuka taarifa kuwa klabu ya Coastal Union, inayoshiriki ligi kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, imewatimua wachezaji wake wawili Haruna Moshi
‘Boban’ na Juma Said ‘Nyoso’.
Kwa mujibu wa Katibu wa Coastal Union,
Kassim Siagi taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani bado klabu ina
mkataba na wachezaji hao.
Kumezuka maneno yasiyo na ithibati katika mitandao ya kijamii na baadhi
ya vyombo vya habari hasa baadhi ya magazeti kuwa wachezaji hao
wametimuliwa kikosini kutokana na vitendo vya hujuma wakiwahusisha na
kucheza chini ya kiwango katika mechi dhidi ya Azam FC, iliyoisha kwa
Wagosi kulala 4-0.
Baada ya hapo ikadaiwa wachezaji hao wametemwa,
lakini ukweli ni kuwa kocha wa Coastal Union, ameamua kuwatumia viajana
wa kikosi cha pili na baadhi ya wachezaji ambao walikuwa nje kwa muda
mrefu.
Maamuzi hayo ya kocha Yusuf Chipo, ni kwa lengo la
kuhakikisha Coastal Union inakuwa na sura mpya huku akiendelea kuwatumia
wachezaji wakongwe walio katika klabu hiyo kwasababu ya uzoefu.
Kwa
mara ya kwanza kutumiwa kwa mfumo huo mpya ilikuwa ni katika mechi
dhidi ya Simba katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, ambapo
wagosi waliibuka na ushindi finyu wa bao 1-0 lililoingizwa kimiani na
beki wa kulia Hamadi Juma.
Hivyo ieleweke kuwa wachezaji waliotajwa
kutimuliwa bado ni wachezaji halali wa Coastal Union na wataendelea
kutumika katika mechi nne zilizobaki kwa utaratibu aliouweka kocha.
Angalizo:
Si vema kuzungumza habari ambazo hazina uhakika, namba ya simu
ya msemaji ni 0713 593894. Muda wowote ukiwa na kitu kinakukwaza
usichoke kuuliza kwa ufafanuzi Zaidi.
HAFIDH KIDO
MSEMAJI- CUSC.
28 March 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment