Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 April 2014
Sunday, April 06, 2014

LEWANDOWSKI AMEJEREA KUIVAA REAL MADRID



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Kiungo wa Ujerumani, Marco Reus ameungama kuwa Borussia Dortmund watatakiwa kuongeza bidii ili waweze kupindua kichapo cha 3-0 watakapo waalika miamba wa Uhispania, Real Madrid, katika mechi ya marudiano ya robo fainali yao ya kombe la mabingwa Jumanne.

Real waliwanyuka miamba hao wa Ujerumani kwa urahisi kwenye uwanja wao wa Bernabeu Jumatano iliopita huku nyota wao, Gareth Bale, Isco na Cristiano Ronaldo, wakipata magoli hayo.

Staa wa Poland Robert Lewandowski, ambaye alitumikia adhabu katika mkondo wa kwanza, atarejea wakati Dortmund watakapo wakaribisha Real katika uwanja wao wa Westfalenstadion. 

Lewandowski alizamisha magoli manne wakati mafahari hao walipomenyana msimu uliopita katika semi-fainali ya shindano hilo na alionyesha makali yake pale alipofunga la uamuzi katika ushindi wao wa 2-1 kwenye ligi ya Ujerumani, Bundesliga, Jumamosi dhidi ya VfL Wolfsburg. 

“Hatujakufa moyo bado na tukicheza kama kipindi cha kwanza (dhidi ya Wolfsburg), itakuwa vigumu lakini tukiweza kujidhihirisha kama cha pili, tuna nafasi kubwa,” Reus alisema.
“Itakuwa kibarua kigumu lakini tutajaribu lolote liwezekanalo,” aliendelea.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!