MICHAEL CARRICK ALETA AMSHA AMSHA UNITED.
Kiungo Michael Carrick ameshinikiza wenzake waicharaze West Ham katika ligi ya Premier ili kuonyesha ushindi wao dhidi ya Olympiakos kwenye kombe la klabu bingwa barani Uropa kati kati mwa juma haukua mwanzo mpya wa badia.
United wamedorora katika msimu wao wa kwanza chini ya uongozi wa David Moyes huku wakizama zaidi pale walipo pepetwa na maasimu wao Liverpool 3-0 nyumbani kwao Old Trafford juma lililopita.
Huku kila mmoja akiwasilisha rambi rambi zao, United walijikakamua na kufuta ushindi wa 2-0 dhidi ya Olympiakos na kushinda 3-2 kwa ujumla katika mkondo wa pili wa mechi yao ya raundi ya 16-bora kufuzu robo fainali ya Champions League.
Ikisalia mechi tisa kabla ya kufunga msimu wa Premier, United wamo alama 12 nyuma ya nafasi nne bora na kiungo huyo wa kati amewahimiza wenzake waaamke na kudhihirisha makali yao.
“Natumahi ushindi huo (OLympiakos) utatupa imani na ujasiri kuzindua mwamko mpya dhabiti.
Hapo awali, tumejipata kwenye hali hii lakini tukashindwa kujimudu na matokeo ambayo hatutarajii.
“Kuna mechi dhidi ya West Ham Jumamosi na ile ya Manchester City Jumanne kutafakari na ni wakati bora kuonyesha ukakamavu wa kupata uzoefu wa kuandikisha matokeo mema,” Carrick alisisitiza.
Kiungo wao mpya, Juan Mata, huendaa akarejea baada ya kukosa mechi ya Olympiakos kwa sababu za kisheria kwani aliwahi chezea Chelsea katika shindano hilo awali msimu huu.
0 comments:
Post a Comment