Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 March 2014
Friday, March 21, 2014

ROONEY ASEMA"MSITUCHUKULIE POA"



Nyota Wayne Rooney ameonya wapinzani wao kwenye kombe la klabu bingwa barani Uropa kwamba makali ya Manchester United bado yapo baada ya miamba hao wa Uingereza kujikatia tiketi ya robo fainali. 

Ingawa United, mabingwa wa Uingereza, waliaga mashindano ya Premier, kombe la FA na lile la Capital One mapema, wamesalia kukita matumaini ya kushamiri na kinyang’anyiro hicho kikuu zaidi ili kuokoa msimu wa ndoto mbaya chini ya utawala mpya wa meneja David Moyes. 

Magwiji hao walifuta kunyukwa mabao mawili ugenini Olympiakos na kufuzu 3-2 kwa ujumla baada ya kuwachakaza mabingwa hao wa Ugiriki 3-0 nyumbani kwao Old Trafford kwenye raundi ya 16-bora ya Champions League Jumatano. 

“Katika shindano la kombe, chochote chaweza kutokea. Tumefuzu robo fainali na lolote linawezekana kutoka hapo. Vilabu vitatu vya Hispania vilivyo salia ni mahiri, Chelsea wanacheza soka ya hali ya juu na bila shaka, mabingwa Bayern Munich bado wapo.
“PSG (Ufaransa), pia wametamba na yeyote tutakaye mpata itakuwa ni kibarua lakini tuko tayari kupambana,” straika huyo wa Uingereza aliyeunganisha mabao mawili kati ya matatu yaliofungwa na mwenzake Robin Van Persie, alisema. 

Kwa sasa, United wanatazamia ushindi huo kusitiri shutuma kali dhidi ya Moyes utawasismua kumaliza ligi ya Premier kwa kishindo, kuanzia Jumamosi watakapo menyana na West Ham United.
Rooney na wenzake wameshikilia kuwa matumaini ya kumaliza miongoni mwa timu nne bora bado yapo licha ya mwaya mkuu wa pointi 12 kutoka watanashari wao Manchester City.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!