Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 March 2014
Friday, March 21, 2014

GAEL CLICHY ASEMA KOMBE WALILOPATA HALITOSHI




Beki wa Machester City, Gael Clichy amekiri kukosa kunyakua taji la ligi ya Premier ya Uingereza ni wazo ambalo wana Manchester City hawatakubali huku wakijiandaa kukutana na Fulham Jumamosi.
Tayari City wametia kombe la League Cup kibindoni lakini harakati zao za kuwania vile vya FA na Champions League zilifikia kikomo mikononi mwa Wigan na Barcelona. 

Clichy amesema kuwa ni wakati wa kutia matokeo hayo duni kwenye kaburi  na kuganga yajayo ili waweze kunyakua taji pekee wanalowania msimu uliosalia.
“Kushinda Capital One pekee hakuridhishi. Ikiwa huna hamu ya kushindania mechi zote kwa ujasiri liwalo liwe, basi huna nafasi hapa City. Wakati umewadia wa kupigania alama zote tukianzia na Fulham kwani tuna bahati ya kuwa kwenye kikosi staid. 

“Tuna jukumu la kuwazawadia mashabiki wetu wapendwa taji hili lakini bado, haliko mfukoni,” beki huyo wa kushoto wa Ufaransa alinena.
City wanaketi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ya Premier ingawa wana mechi tatu za ziada ambazo wakifanikiwa kuzishinda, watakuwa wamiliki wa nafasi ya kwanza. 

Walishinda taji hilo mara ya mwisho msimu wa 2011/12 baada ya kuwaandama maasimu wao wa jadi, Manchester United kabla ya kuwapokonya ushindi sekunde za mwisho za kampeni hiyo.
“Tulionja utamu wa ushindi miaka miwili iliyopita na ninahimiza wenzangu tujikaze ili kurudia hali hiyo. Ikiwa tutaendelea kushinda kama vile tulifanya dhidi ya timu ya Hull, basi kombe litakuwa letu,” beki huyo huyo aliongeza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!