Home
»
Unlabelled
» STARS INAHITAJI KIKAO NA ENGLAND,SOUTH AFRICA.
By Oscar Oscar Jr
Uingereza pamoja na ukubwa wao,umaarufu wao,ubora wa EPL lakini
ukiwapeleka EURO au Kombe la Dunia ni vichapo tu!! Kuna kipindi ilibaki
kidogo tu,wangesema ukitoa MESSI na CR7,WILSHERE ndo anafuata!!
South Africa nao ndo wale wale,wanapumulia mitambo.SA ya kuanzi kwa
kina Mark Fish na Siyabonga Nomvete hadi hapa kwa kina Parker na
Tshabalala utagundua kwamba,hawana lolote.
TAIFA STARS
inahitaji zaidi ya kuwa na ligi bora,viwanja vizuri na vifaa pia.Wakati
namuona SAID BAHANUZI kwa mara ya kwanza akiwa na YANGA,nilidhani jamaa
anatoka Afrika Magharibi!!
Baada ya camera kumuandama,sasa ameamua kutafuta kwanza liboni za kuvaa mkononi,mpira atacheza baadae!!!
Tunahitaji kikao na Uingereza na Afrika kusini watueleza kwa nini
hawafanikiwi wakati sisi tunadhani,tukiwa kama wao tutashinda kombe la
Dunia.
0 comments:
Post a Comment