NIONAVYO MIMI KWA MAN UNITED
kocha David Moyes anaweza pata mafanikio akiwa na kikosi cha United lakini asimwamini sana Rio Ferdinand na keptain wake Vidic.Rio amecheza vizuri sana msimu uliopita na kwa umri anaweza kupata pancha muda wowote.Vidic naona majuruhi yamekuwa yanamwandama na nadhani yakiendelea,basi siku zake zitaanza kuhesabika.
Moyes anataka kuimarisha safu ya kiungo kwa kutupa ndoano kwa Alcantara na Fabregas ambako dalili zinaonyesha atafeli.Mi ningemshauri amwangalie Adel Taarabt wa QPR na Ben Arfa wa newcastle nadhani jamaa wanaweza msaidia.
Unapokuwa na Hatem Ben Arfa unaongeza mtu mwenye kasi na akili kwenye timu na kuna uwezekano akapatikana sio kwa bei kubwa sana ingawa Magpies hawatokubali kirahisi.Adel Taraabt shughuli yake sio ya kitoto na sidhani kama anaweza kuikataa timu kubwa kama united.
Nimewataja Ben Arfa na Taarabt kwa sababu,wanaweza wote kucheza kwenye Dimba na pembeni mwa uwanja ambako pia Nani,Young na Valencia wamekuwa kama homa za vipindi kuna muda wanafanya vizuri na kuna wakati wanavurunda.
Man united wanaweza kuongeza wachezaji wa kiwango cha kati tu kama wawili na Gari likashika kasi,wakati mwingine kuwahitaji kina Ronaldo na Gareth Bale ambao wanagharama kubwa mno,naona kama ni siasa tu.
0 comments:
Post a Comment