Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 July 2013
Sunday, July 21, 2013

NIONAVYO MIMI HUU NI "USHABIKI MBUZI"


Baada ya Kelvin Yondani kuachana na Club yake ya simba na kujiunga na club ya Yanga,mechi yake ya kwanza dhidi ya Simba alichezewa rafu mbaya kabisa na Haruna Moshi Boban ya makusudi.

Baada ya tukio hilo la kusikitisha,upande wa mashabiki wa msimbazi walionekana kufurahi na kuchekelea kile alichokifanya Bobani kwa Yondani,eti ni kwa sababu Yondani ni msaliti kwa hiyo acha afe tu!

Mechi ya mwisho ya msimu uliokwisha,kiungo wa Yanga Nizar Khalfani kuna muda alipiga bonge la shuti kwenda kwa Juma Kasseja na kwabahati Mbaya mpira ule ulimfanya Kasseja ajigonge kwenye bomba la goli na kuumia.

Cha ajabu wakati kasseja akiugulia chini mashabiki wa Yanga walikuwa wakichekelea na kumzomea!!!

Hebu tuwe na akili,hivi Kasseja akifa uwanjani we shabiki wa Yanga unapata faida gani?? Baada ya Tito Villanova kujiuzulu nafasi yake,ukimsikiliza kocha wa Madrid Carlo Anceloti unaweza sema yeye na Tito ni watoto wa baba mmoja kwa namna ugonjwa wa Tito unavyomgusa.

Najua vurugu za watani wa jadi hata ulaya zipo lakini sio lazima kila kinachotokea Ulaya kitokee na Tanzania na pia,ulaya wanaonyesha heshima sana mchezaji akiumia bila kujali ni wa timu gani LETS DO THIS!!

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!