Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 January 2015
Tuesday, January 20, 2015

Yaya Toure amwaminia kocha


Na Chikoti Cico

Kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester City Yaya Toure ana amini kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coast Herve Renard ataiwezesha timu hiyo kushinda mchezo wa kundi D dhidi ya Guinea utakaochezwa leo jioni na pia kuifikisha timu hiyo mbali kwenye michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika inayofanyika nchini Guinea ya Ikweta.

Mchezo huo ambao utakuwa ni wa ufunguzi wa kundi D unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Estadio de Malabo huku timu ya Ivory Coast ikipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.

Kuelekea mchezo huo Toure alisema “kabla sijastaafu hakika nataka kushinda kitu na nchi yangu, nina ujasiri kwamba Herve Renard atatupeleka mbali iwezekanavyo, ni mtu ambaye ana uzoefu sana wa Afrika, ni mtu mwenye haiba nyingi na anajua nini kinahitajika ili kushind”

Kuelekea mchezo huo wa Ivory Coast dhidi ya Guinea takwimu zinaonyesha timu hizi mbili zimekutana mara 15 katika mashindano huku Ivory Coast ikishinda michezo 10 na kufungwa michezo mitatu huku wakitoka sare michezo miwili.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!