Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 January 2015
Monday, January 19, 2015

Kevin Mirallas ainyima ushindi Everton.


Na Chikoti Cico

Mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza kati ya Everton dhidi ya West browmich Albion uliochezwa usiku wa Jumatatu uliisha kwa matokeo ya sare ya bila kufungana kati ya timu hizo mbili huku ukiwa mchezo wa sita bila ya ushindi kwa timu ya Everton.

Pamoja na kwamba kila timu ilipata alama moja kutokana na sare hiyo lakini kitendo cha kiungo wa Everton Kevin Mirallas kung’ang’ania kupiga penati ambayo alikosa kwenye dakika ya 43 kwa kumnyanga’nya mpira Leighton Baines ambaye ndiye mpigaji wa siku zote kwa timu ya Everton kiliibua mshangao mkubwa kwa mashabiki wa Everton.

Kitendo hicho ambacho Gary Neville alikiita “dharau” huku Jamie Carragher akikiita “ubinafsi” na kwa kocha wa Everton Roberto Martinez alisema ni “bahati mbaya”. Lakini kwa ujumla ni kitendo kilichosababisha Everton wasipate goli ama ushindi kwenye uwanja wao wa Goodison Park.

Baines ambaye ana rekodi ya kufunga penati 15 kati ya 16 alizopiga alibakiwa na mshangao baada ya Mirallas kulazimisha kupiga penati hiyo kitendo kilichosababisha klabu ya Everton kubaki nafasi ya 12 huku wakikiwa na alama 23.

Wakati huo huo kocha wa West Brom Tony Pulis mpaka sasa amejikusanyia alama nne katika michezo miwili aliyocheza toka alipochukua jukumu la kuifundisha klabu ya West Brom mapema mwezi huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!