Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 January 2015
Tuesday, January 20, 2015

Figo awaongelea Ronaldo na Messi.


Na Chikoti Cico

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno ambaye alizichezea timu zote mbili za Barcelona na Real Madrid, Luis Figo awaongelea Christiano Ronaldo na Lionel Messi na kudai miaka 15 iliyopita wasingeweza kuwika kama sasa wanavyowika.

Figo anadhani kwamba Ronaldo na Messi ambao kwasasa ndiyo wachezaji ambao wana viwango bora duniani huku wakivunja rekodi za magoli kila mara anaamini ingekuwa ngumu kwa wachezaji hawa wawili kufanya hivyo kama wangekuwa wanacheza miaka 1990 na 2000.

“Kama ningekuwa kocha ningejaribu kuwasajili Messi ama Christiano, wachezaji wawili bora ambao wako juu kuliko wengine. Lakini nilikuwa na bahati ya kutosha kucheza na wachezaji bora kwenye timu yangu pamoja na wapinzani ambao kabisa inawezekana walikuwa hata zaidi ya Christiano na Messi” aliyasema hayo Figo.

Mchezaji huyo ambaye aliwahi pia kuichezea Inter Milan alizungumzia pia timu zinazoweza kunyakua kombe la ligi ya mabingwa Ulaya na kusema “kombe la ligi ya mabingwa? Huu utakuwa mwaka wa mojawapo kati ya Real Madrid, Barca, Bayern, Chelsea…”

Pia akiongelea kuhusu mbio za ubingwa kwenye ligi kuu nchini Hispania maarufu kama “la liga” alisema “la liga? Kuna utawala yakinifu kwa timu mbili zenye nguvu kidesturi, Barca na Real Madrid”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!