Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 January 2015
Tuesday, January 20, 2015

Mourinnho awakataa Falcao na Di Maria.


Na Chikoti Cico

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anadai alikataa kuwasajili Radamel Falcao na Angel di Maria kwenye kipindi kilichopita cha majira ya joto kutokana na mishahara yao kuwa mikubwa kitu ambacho kingeleta hali ya sintofahamu miongoni mwa wachezaji wengine ndani ya klabu ya Chelsea.

Mourinho ambaye wakala wake Jorge Mendes pia anawawakilisha Falcao na Di Maria anadai alipewa nafasi ya kuwasajili wachezaji hao kabla ya Manchester United kuwasajili ambapo Falcao alisajiliwa kwa mkopo wa mpaka mwisho wa msimu akitokea Monaco huku Di Maria akisajiliwa kutoka Real Madrid kwa rekodi ya pauni milioni 60.

Katika kitabu kipya cha “The Key to Mendes” Mourinho akiongelea kwanini alikataa kuwasajili wachezaji hao alisema “siweza kuwa na mchezaji anayelipwa Euro milioni 10 wakati wengine wanalipwa tatu, nne ama tano, hilo lingesababisha mlipuko”

Mshambuliaji wa Manchester United Mcolombia Radamel Falcao anapokea mshahara wa pauni 265,000 kwa wiki huku Di Maria akipokea pauni 200,000 kwa wiki, mishahara ambayo Mourinho anasema ingeleta “mlipuko” kati ya wachezaji wa Chelsea kama timu hiyo ingewasijili.

Aliendelea kusema “Jorge (Mendes) aliniambia Di Maria na Falcao ni wachezaji wake na anatakiwa kutafuta suluhisho kwaajili yao. Lakini kama Chelsea hawana uwezo wa kifedha kulipa Euro milioni nane, tisa, 10 kwa mwaka kwasababu ya mchezo wa kiungwana (Fair Play) hivyo Mendes inabidi afikirie kuhusu wachezaji wake”.

Mourinho alitumia kiasi cha pauni milioni 88 kuwasajili Cesc Fabregas, Diego Costa, Filipe Luis na Loic Remy kwenye kipindi kilichopita cha majira ya joto huku sehemu kubwa ya fedha za usajili zikitoka katika mauzo ya David Luiz kwa PSG kwa pauni milioni 50, Romelu Lukaku kwenda Everton kwa pauni milioni 28 na Demba Ba kwenda Besiktas kwa pauni milioni 4.7

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!