Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 January 2015
Monday, January 19, 2015

Fabregas aweka rekodi EPL.


Na Chikoti Cico


Kiungo wa klabu ya Chelsea Cesc Fabregas ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya ligi kuu nchini Uingereza kufikisha pasi 15 za magoli (assists) ndani ya misimu miwili.

Kiungo huyo ambaye alijiunga na klabu ya Chelsea wakati wa majira ya joto akitokea klabu ya Barcelona mpaka sasa amefikisha “assists” 15 kwenye michezo 22 toka kuanza kwa msimu wa 2014/2015, Fabregas alifikisha “assist” ya 15 kwenye mchezo dhidi ya Swansea ambapo Chelsea ilishinda kwa magoli 5-0.

Fabregas ameweka rekodi hiyo tangu alipoanza kuichezea klabu ya Arsenal kwenye msimu wa mwaka 2007-2008 ambapo alifikisha “assist” 17 ingawa klabu hiyo inayofundishwa na kocha Arsene Wenger ilimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Chelsea na mabingwa Manchester United kwenye msimu huo.

Wakati huo huo Fabregas anakaribia kuifikia rekodi ya “assists” 20 iliyowekwa na Thierry Henry ndani ya msimu mmoja wa mwaka 2002-2003 wakati akiichezea klabu ya Arsenal.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!