Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 January 2015
Monday, January 26, 2015

Costa mwingine aitaka Chelsea




Na Chikoti Cico


Wakati dirisha dogo la usajili likikaribia kufikia mwisho klabu ya Chelsea imeendelea kusaka saini ya kiungo wa Shakhtar Donetsk Douglas Costa ambaye ameonyesha nia ya kutaka kujiunga na klabu hiyo yenye maskani yake jijini London.

Chelsea ambayo ofa yake ya mara ya kwanza ya pauni milioni 16 ilikataliwa na klabu ya Shakhtar imeongeza ofa hiyo na kufikia pauni milioni 18.7 zikiwa ni taarifa kutoka kwa kiungo hiyo ambaye anataka kucheza chini ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho.

Costa akiongea na mtandao wa GloboESporte.com kuhusu nia yake ya kutaka kucheza chini ya Mourinho alisema “kucheza Chelsea ni ndoto kwa mchezaji yeyote, inasimama karibu na baadhi ya wachezaji bora duniani na inashindana na walio bora pia lakini hakika kilichonivutia machoni ni kocha. Ni kocha mwerevu na amekuwa mshindi kila alipoenda, kitu ambacho kitanipa furaha sana kucheza kwa Chelsea kitakuwa hiki.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye amecheza kwa miaka mitano chini ya kocha wa Donetsk, Mircea Lucescu anaamini Mourinho atafikisha soka lake kwenye ngazi ya juu zaidi.

Costa aliendelea kusema “nimejifunza mengi na Lucesc, niliwasili Shakhtar katika umri wa miaka 19 na amenifundisha mengi, nina shukuru sana lakini pia najua na Mourinho pale Chelsea maendeleo yangu yatakuwa makubwa zaidi, ameshinda karibu vitu vyote ni sehemu ya walio bora kama sio bora, yuko juu”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!