Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 January 2015
Monday, January 26, 2015

Drogba anyakua tuzo Uingereza.




Na Chikoti Cico


Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Didier Drogba amepewa tuzo ya heshima na chama cha Waandishi wa mpira wa miguu (Football Writers Association) cha nchini Uingereza katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Savoy jijini London siku ya Jumapili.

Drogba amepewa tuzo hiyo ya heshima na chama cha Waandishi wa Habari kwa kutambua mchango wake kwa timu ya Chelsea na ligi kuu nchini Uingereza kwa zaidi ya miaka 16 lakini pia kazi zake za jamii kupitia shirika lake ambalo limetoa mchango mkubwa kwenye miradi mbalimbali ya jamii nchini Ivory Coast.

Drogba akiongea baada ya kupokea tuzo hiyo alisema “ hakika ninajivunia kwa tuzo hii, katika orodha ya washindi waliopita kuna wachezaji wengi ambao hakika ninawaheshimu na nilikua nikijaribu kufikia ngazi zao kwahiyo kwangu hii ni heshima kubwa”.

“Wakati nilipokuja Uingereza mambo yalikuwa magumu kulikuwa na vizuizi vya lugha na kubadilika kwa utamaduni. Baada ya muda tuliweza kujifunza zaidi kutoka kwa kila mmoja na leo ninafuraha kwamba waandishi wa soka sio tu wamenielewa mimi sana uwanjani lakini pia wamenisaidia na kazi zangu za shirika”.

Naye kocha wa Chelsea Jose Mourinho mapema akimwongelea Drogba na “Football Writers Association” alisema “nilikuja Chelsea wakati wa majira ya joto ya mwaka 2004 na taarifa yangu ya kwanza kwa Mr Abramovich kuhusiana na mipango yangu kwa klabu, nilitoa majina ya baadhi ya wachezaji”

“Majina makubwa yaliwasili Chelsea kwenye kipindi hicho, majira ya joto yaliyopita kwa mfano Claude Makelele alikuja kutokea Real Madrid na Hernan Crespo alikuja kutoka Inter wachache kati ya wengi lakini Drogba alikuwa hajulikani na bei ilikuwa kubwa  sana ila bado nilijua kwa usahihi kama nilivyowahi kufanya kwamba alikuwa mchezaji niliyemtaka”

Aliendelea kusema “Nilikuwa shupavu kushinikiza klabu yangu kulipa kiasi hicho kwaajili yake na nadhani tayari tunaweza kusema alikuwa usajili bora wa thamani kwa Chelsea kuhusiana kwa ambacho amekifanya kwa klabu hii kwa miaka mingi na bado hajamaliza”

Drogba anaungana na Jose Mourinho, Sir Alex Ferguson na David Beckham ambao walishawahi kuchukua tuzo hiyo ya heshima.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!