Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 January 2015
Tuesday, January 27, 2015

Leo ni Chelsea vs Liverpool (saa 4:45 usiku)



Na Chikoti Cico

Baada ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Capital One kati ya Liverpool dhidi ya Chelsea uliopigwa wiki moja iliyopita kwenye uwanja wa Anfield kuisha kwa sare ya goli 1-1, usiku wa leo timu hizo mbili zitarudiana tena kwenye uwanja wa Stamford Bridge katika nusu fainali ya pili ya Capital One.

Chelsea ambao wametolewa kwenye kinyang’anyiro cha kombe la FA baada ya kufungwa kwa magoli 4-2 na klabu ya Bradford City kutoka ligi daraja la kwanza inatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kwa nguvu zote ili kutafuta ushindi na kuingia fainali.

Kwenye mchezo huo kocha wa Chelsea Jose Mourinho anatarajiwa kuchezesha kikosi chake cha kwanza ambacho kitakuwa tofauti na kikosi kilichocheza walipofungwa na Bardford hivyo nahodha John Terry, kipa Courtois, Branislav Ivanovic, Nemanja Matic, Diego Costa, Cesc Fabregas, Eden Hazard na Willian wanatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza.

Kuelekea mchezo Mourinho amewataka wachezaji wa Chelsea kusahau machungu ya kutolewa kwenye kombe la FA na kulenga zaidi mchezo huo dhidi ya Liverpool.

“mwishoni mwa Mei hatutaenda Wembley kucheza fainali ya kombe la FA hiyo ni hakika. Kombe la FA limeisha kwetu, hatutaenda pale hata kucheza nusu fainali ya kombe la FA. Limeishwa kwetu”

“Kwenda pale nadhani hilo litakuwa na maana zaidi kwa kila mtu-nafasi ya mwisho tuliyonayo ni hii moja kucheza pale kwenye fainali ya kombe la Capital One” alisema Mourinho.
 
Nayo klabu ya Liverpool ambayo kwenye mchezo wa kwanza ilionyesha kandanda safi pamoja na kutoka sare ya goli 1-1- inatarajiwa kupigana kufa na kupona ili kuweza kushinda mchezo huo wa nusu fainali na kuweza kuingia fainali itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley.

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anatarajiwa kuwarejesha kikosini kiungo Steven Gerrard na beki Martin Skrtel ambao walipumzishwa kwenye mchezo wa raundi ya nne wa kombe la FA dhidi ya Bolton uliochezwa mwishoni mwa wiki.

Pia kuna taarifa kwamba mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge ambaye alikuwa nje toka mwezi Agasti anaweza kucheza mchezo huo.

Brendan Rodgers akiongea kuelekea mchezo huo amesema “tunawaheshimu wapinzani ni kweli kwasababu ni timu nzuri lakini hatuna cha kuogiopa kwenye mchezo.

Sisi ni timu ammbayo ipo kwenye wakati mzuri, tunacheza vizuri, tunafanya kazi vizuri na tunajua tunaweza kwenda pale na kushinda, hilo ndiyo muhimu”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!