Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Juan Mata anajiandaa kupigwa bei.


Na Oscar Oscar Jr

Pamoja na ubora ambao amekuwa akiuonyesha kila anapopata nafasi, kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Juan Mata anaweza kuonyeshwa mlango wa kutokea pale Old Trafford mwishoni mwa msimu huu kama atashindwa kuonyesha kiwango cha kumridhisha kocha Loius Van Gaal.

Klabu ya Sevilla inatajwa kutaka kumrejesha kiungo huyo kwenye ligi ya Hispania mahali ambako ulimwengu ulimtambua lakini inadaiwa kuwa itakuwa ngumu kwa Manchester United kumuachia mchezaji huyo kabla ya kununua mbadala wake.

Mata ambaye aliuzwa na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kwenye dirisha dogo msimu uliopita, amekuwa kwenye wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kufuatia Muhispania huyo kucheza namba moja na nahodha wa timu hiyo, Wayne Rooney.

Kocha wa Manchester United, anamnyatia kiungo wa klabu ya Roma, Kevin Strootman, na endapo atampata basi uwezekano wa Juan Mata kupigwa bei ni mkubwa mno.

Mata ndiye aliyefunga bao la ushindi kwa United kwenye mchezo wao wa siku ya jumanne usiku ambao waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Stoke City kwenye dimba la Old Trafford.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!